DALILI ZA KUKATAZA PICHA
DALILI ZA KUKATAZA
KUPIGA PICHA
NA KUTUMIA PICHA.
AMEANDIKA
SHEIKH ABUL YAMAAN ADNAAN
BIN HUSSEIN MMASQARY
ALLAH AMUHIFADHI
DARUL HADITH DAR ES SALAAM
KITABU NA SUNNA KWA
UFAHAMU WA WEMA
WALIOTANGULIA.
بسم الله الرحمن الرحيم.
Sifa zote njema ni za Allah subhana wataala na sala na salamu ziwe juu ya mtume wake ض n,ama baada;hizi ni baadhi ya dalili za kuharamisha picha na kutumia picha bila ya dharura yoyote wamezikadiria watu wa elimu sawa sawa katika kinyago au photographiya au zinginezo,nimeifupisha katoka katika maneno ya shekhe wetu muqbil allah amrehemu na nimeziunganisha na fatawa za shekhe ibn bazz na lajnatu addaaimah na shekhe albaany allah awarehemu na awasamehe.
AMELAANI MTUME ض MPIGA PICHA
-
Kutoka kwa aun bin abi juhfah kutoka kwa baba yake yakuwa yeye alinunua kijana mpiga chuku akasema yakuwa mtume ضalikataza kutokana na thamani ya mbwa(yaani kuuza) na chumo la malaya na akalaani mla ribaa na mwenye kuitoa na mwenye kuchora tatoo na mchorwaji na mpiga picha.amepokea bukhary
-
Maamrisho ya kuchana picha:kutoka kwa abi alhayyaj al-asady amesema ameniambia ally bin abi twaalib:je nisikutume yale ambayo amenituma nayo mtume wa allah:usiache picha isipokuwa uichane wa kaburi lilonyanyuliwa isipokuwa uliweke sawa.amepokea muslim na katika riwaya na wala sura isipokuwa uichane.
-
PICHA HUWENDA IKAABUDIWA ASIOKUWA ALLAH.
-
Na kutoka kwa aisha amesema pindi alipoumwa mtume walitaja baadhi ya wake zake mtume kanisa waliliona katika ardhi ya habash linaitwa mariya na alikuwa ummu sulaim na ummu habibah walitoka ardhi ya habash wakataja uzuri wake na picha ziliyomo katika kanisa hilo,akainuwa kichwa mtume akasema hakika hao akifa miongoni mwao mtu wema wanajengea juu ya kaburi lake msikiti kisha wanachora humo picha hizo,hakika hao ni viumbo waovu mbele ya allah.amepokea bukhary na muslim.
-
Malaika hawaingii nyumba ambayo ina picha.
-
Na kutoka kwa ibn abbas kwa abi twalha amesema amesema mtume malaika hawaingii nyumba ndani yake kuna mbwa wala picha.amepokea bukhary na muslim.
-
Kutoka kwa abi twalha swahaba wa mtume amesema mtume amesema hakika malaika hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna picha.ameipokea bukhari.
-
Kutoka kwa ibn omar amesema alimuaidi jibril mtume akachelewa =================akatoka mtume akakutana nae akamshtakia kile alichokipata katika nafsi yake akamuambia hakika sisi hatuingii nyumba ambayo ndani yake kuna picha au mbwa.amepokea bukhary
-
Kutoka kwa kwa aisha yakuwa yeye amesema:alimuaidi mtume wa allah jibiril juu yake salamu katika saa amjie ukawadia ule mda na hakumjia na mtume wa allah fimbo iko mikononi mwake akaitupa na akasema hakuwa allah mwenye kukhilifu ahadi yake wala mtume wake(jibriil)kisha akageuka tahamaki kuna ka mbwa chini ya kitnda akasema ewe aisha saa ngapi ameingia mbwa hapa?akasema naapa kwa jina la allah sijui, akaamrisha akatolewa akaja jibril akasema mtume wa allah “umeniahidi nikakaa kwa ajili yako na haujaja?”akasema amenikataza mimi mbwa ambae alikuwa ndani kwako ,hakika sisi hatuingii nyumba ambayo kuna mbwa wala sura.ameipokea muslim
-
Kutoka kwa aisha yakuwa yeye alinunua kitambaa chenye picha akasimama mtume wa allah na hakuingia ,nikasema natubu kwa allah nimetenda dhambi gani?akasema ni kipi kitambaa hiki?nikasema ili ukalie na kushoneshee mito akasema “hakika watengenezaji wa picha hizi wanaadhibiwa siku ya kiama wanaambiwa huwisheni mlivyo viumba na hakika malaika hawaingii hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna picha.amepokea bukhary
-
Kutoka kwa aisha yakuwa yeye alinunua kitambaa chenye picha pindi alipokiona mtume wa allah akasimama mlangoni na hakuingia ikajulikana au nikajua kuchukia kutoka katika uso wake akasema “ewe mtume wa allah natubu kwa allah na mtume wake nimetenda dhambi gani? ni kipi kitambaa hiki?akasema ili ukalie na kushoneshee mito akasema “hakika watengenezaji wa picha hizi wanaadhibiwa siku ya kiama wanaambiwa huwisheni mlivyo viumba na hakika nyumba ambayo ina picha haiingiwi na malaika.amepokea muslim
-
Kutoka kwa ibn abbas anasema amenipa khabari maimunah yakuwa mtume alipambazukiwa siku moja===== akasema maimunah ewe mtume wa allah nimelichukia umbile lako tokea leo ,akasema mtume wa allah “hakika jibriil aliniaidi kukutana usiku wa jana na hakukutana na mi,ama wallah hakuniacha”
-
akasema akashinda mtume siku yake ile juu ya hilo,kisha akingiwa katika nafsi yake kitu tahamaki akamuona mbwa chini ya kitanda,akaamrisha atolewe kisha akachukua kitambaa kilioloana akapaosha, pindi aliopofikiwa na mchana akamjia jia jibriil akamuambia “hakika ulikuwa umeniahidi tukutane jana?akasema ndio nilikuahidi lakini sisi hatuingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha ,akapambazukiwa mtume wa allah siku hiyo akiwa mwenye kuamrisha kuuwa mbwa mpaka akawa anaamrisha kuuwa mbwa wadogo wa ulinzi wa shamba na waachwe wakubwa amepokea muslim.
-
Kutoka kwa abi huraira anasema amesema mtume wa allah haingii malaaika nyumba ambayo kuna kinyago au picha.
-
Kutoka kwa ally anasema nilitengeneza chakula kisha nikamuita mtume wa allah akaja,akaona pazia lenye picha akatoka na akasema hakika malaika hawaingii nyumba ambayo kuna mapicha.
-
Kutoka kwa ally anasema nilitengeneza chakula kisha nikamuita mtume wa allah akaja,akaona pazia lenye picha akarudi ,akasema ally ewe mtume wa allah kitu gani kimekurudisha?akasema “hakika ndani ya nyumba kuna pazia lenye picha na kwa hakika malaika hawaingii nyumba ambayo kuna mapicha.amepokea imamu abu yaala
-
MIONGONI MWA WATU WENYE ADHABU KALI SIKU YA KIYAMA WAPIGA PICHA
-
Kutoka kwa abdillah amesema ,nimemsikia mtume wa allah anasema “Hakika watu wenye adhabu kali siku ya kiama wapiga picha”.amepokea bukhary na muslim
-
Kutoka kwa ibn omar hakika mtume wa allah amesema “hakika hawa wanaotengeneza picha hizi wanaadhibiwa siku ya kiyaama wanaambiwa huwisheni mlio viumba”. amepokea bukhary na muslim
WAPIGA PICHA NI MIONGONI MWA maDHWALIM
-
Kutoka kwa abi zur’aa amesema”Niliingia pamoja na Abu Hurairanyumba ya madina ,akaona katika sehemu ya juu ya nyumba hiyo mtengenezaji picha anatengeneza picha akasema,nimemsikia mtume===akisema “Na nani aliye dhalimu zaidi kuliko mwenye kwenda anaumba kama uumbaji wangu ,basi na aumbe mbegu au punje”kisha akaagiza[Abu Huraira] chombo chenye maji akaosha mikono yake mpaka akafika katika makwapa yake,nikasema ewe Abu Huraira ni kitu ulichokisikia kwa mtume ===[yaani namna hiyo ya uoshaji mikono],akasema mwisho wa mapambo. ”. ameipokea bukhary na muslimNa kutoka kwa Aisha ~~~ “Alifika mtume === kutoka safarini na hail ya kuwa mimi nimesitiri kwa pazia yangu juu ya *** yangu yenye picha ,wakati alipoiona mtume wa Allah === akaiharibu na akasema “Watu wenye adhbu kali siku ya kiyama ni wale ambao wanafananisha kuumba kwa Allah”anasema Aisha tulikifanya kuwa mto au mito miwili Na kutoka kwa Aisha ~~~ amesema “alifika mtume === kutoka safarini hali ya kuwa nimesitiri mlango wangu kwa pazia yenye picha ya farasi mwenye mbawa akaniamrisha nikaitoa. ameipokea muslimNa kutoka kwa Aisha ~~~ amesimulia,kwa hakika mtume ===aliingia kwake……..kisha akainama kulielekea pazia kisha akalichana kwa mkono wake KATAZO LA KUTENGENEZA PICHA
-
Na kutoka kwa Aisha ~~~ anasema “Aliingia kwangu Mtume === hali ya kuwa nimesitiri mlango wangu kwa pazia yenye picha pindi alipoiona akaichana ukabadilika uso wake,kisha akasema “Ewe Aisha watu wenye adhabu kali zaidi siku ya kiyama ni wale wenye kufananisha na uumbaji wa Allah”Amesema Aisha “tukalikatakata tukalifanya mto au mito miwili.
-
Na kutoka kwa Aisha ~~~ amesema “aliingia mtume === hali ya kuwa nimeweka pazia yenye picha ukabadilika uso wake kisha akaichukua na kuichana kisha akasema “Hakika miongoni mwa watu wenye adhabu kali zaidi siku ya kiyama ni wale wenye kufananisha na uumbaji wa Allah”
-
Amesema Bukhari Allah amrehemu na kutoka kwa Aisha amesema “Alifika mtume=== kutoka safarini na nilitundika **** ina picha akaniamrisha niitoe nikaitoa.
-
DALILI JUU YA UHARAMU WA PICHA ZOTE ZA VIUMBE HAI
-
Kutoka kwa jaabir,amekataza mtume wa allah kuhusu picha inayokuwa imebandikwa kwenye ukuta na akataza kufanya hivyo.amepokea tirmidhy
-
Hadith hii ni hasan nayo iko katika musnad ahmad,na kutoka kwa jaabir bin abdillah hakika mtume wa allah amekataza picha inayo bandikwa ndani ya nyumba na amekataza kufanya hivyo,na kutoka kwa mtume alimuamrisha omar bin khatwaab zama za kufunguliwa makkah na hali yakuwa yuko bat-haa aende kaabah afute kila picha ,na hakuingia kaaba mtume wa allah mpaka zilipofutwa kila picha.ampokea imam ahmad.
-
Kutoka kwa jaabir bin abdillah anadai kuwa mtume wa allah alikataza picha kuwekwa ndani ya nyumba na likataza mtu kufanya hivyo na yakuwa mtume alimuamrisha omar bin khatwaab khatwaab zama za kufunguliwa makkah na hali yakuwa yuko bat-haa aende kaabah afute kila picha ,na hakuingia kaaba mtume wa allah mpaka zilipofutwa kila picha. ampokea imam ahmad
-
Kutoka kwa jaabir bin abdillah anasema hakika mtume wa allah alimuamrisha omar bin khatwaab khatwaab zama za kufunguliwa makkah na hali yakuwa yuko bat-haa aende kaabah afute kila picha ,na hakuingia kaaba mtume wa allah mpaka zilipofutwa kila picha. amepokea imam ahmad
-
Kutoka kwa abi huraira amesema amesema mtume wa allah itatoka shingo toka motoni siku ya kiama shingo hiyo ina macho mawili yanaona na masikio yanasikia na ulimi unaongea unasema:hakika nimewakilishwa kwa vitu vitatu:kila mwenye kiburi mwenye inadi,na kila yule ambaye anadai pamoja na allah muungu mwingine,na mpiga picha.amepokea muslim,tirmidhy.
-
Amesema imam muqbil allah amrehemu katika kitabu chake (hukumu ya kupiga picha viumbe vyenye roho)baada ya kutaja dalili za kukataza jambo hilo:na hizi ni dalili za inajulisha uharamu wa kupiga picha viumbe vyenye roho sawasawa yenye kivuli au zilizokuwa hazina kivuli….etc.\
-
Fatawa ya lajnatu daaimah na bahthi za kielimu na fatawa katika mji wa makkah allah aulinde na miji yote ya kiislam,katika usimamizi wa imam abdul-aziz bin abdillah bin baaz allah amrehemu :kuhusu picha za phptography aksema ni miongoni mwa picha zilizo haramishwa nayo na picha ya kawaida inapita mapito mamoja ================================================================================================================Na kudhihiri picha yangu katika magazeti yangu mawili(itiswaam na fatawa zangu za funga katika mwezi wa ramadhani)sio dalili ya kujuzisha kwangu picha wala kuridhia,hakika mimi sijui wakati wananichukuwa na kunipiga picha…..(na kama inavyojulikana kuwa ibn bazz alikuwa kipofo alikuwa hawezi kujuwa kuwa anapigwa picha ).
-
Na wakasema lajinatu addaima:na wala sio picha====================================================================================================================================================================================================================================================================================================================================================================================================WALHAMDULILLAH RABIL-ALAMIIN
-
-
مرتبط