«

»

HATARI YA TELEVISHENI NA UHARIBIFU WAKE.

HATARI YA TELEVISHENI NA UHARIBIFU WAKE.

Kila sifa njema ni zake Allah na swala na salamu ziwe juu ya mtume wa Allah ﷺ na ahli zake na maswahaba wake na waliokuja baada yao, na nashuhudia ya kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na nashuhudia hakika ya Muhammad ni mja na ni mtume wake.

       Na baada ya utangulizi hakika Allah aliyetukuka ametutahadharisha kutokana na fitina,amesema “ Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Allah ni Mkali wa kuadhibu ”[suratul anfaal:25]

Na amesema aliyetukuka “Basi na watahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo “[An-nuur:63]

     Tambua,na hakika miongoni mwa fitina ambazo zime** zama za mwisho na wamejaribu maadui wa Allah makafiri katika mayahudi na manaswara kuingiza televisheni baina ya waislamu kwa ajili ya kusambaza shari zao na fikra zao kama wanavyotaka ndani ya nyumba za waislamu.

     Na kwa hakika wamefaulu na wame*** juu ya baadhi ya waislamu Allah awaongoze na wamesadikisha maadui hawa dhana yao juu ya waislamu.Kwa hakika wameenda hatua kwa hatua kwa hila chafu,walianza na radio na kanda,kisha wakaingia kwa baadhi ya *** na sinema za pamoja ambazo haziwezi kuonwa isipokuwa kwa hela.

     Kisha wakasambaza televisheni,kisha wakaja na ving’amuzi,na kila kimoja kinachokuja na waislamu wasiokuwa na elimu wanakipinga na wanachuoni wao wanakipinga zaidi.

     Waliendelea mpaka waislamu wakaridhia hayo yote na wakaingiza televisheni na ving’amuzi katika majumba,fikra zao zikabadilika katika kipindi cha muda mfupi na zikabadilika hali zao wakavaa kama makafiri na wakala kama wao na wakanyoa kama wao na wakafanya uzembe kama wao na wakagawanyika makundi makundi na wakafarikiana kama wao.

       Ghafla tumekuwa tunaisha baina ya watu waislamu wanadhihirisha adhana na swala za jamaa lakini mioyo yao haipo pamoja na Allah na pamoja na dini yake.Wamejalia dunia kuwa kusudio lao.

Na *****na hamna hila ya kuacha maasi wala nguvu ya kuelekea mema isipokuwa kwa msaada wa Allah.Enyi waislamu naleta kwenu nyinyi baadhi ya uharibifu wa kifaa hiki ***na swahiba mbaya adui wa ndani na mjumbe wa mayahudi na mfitinishaji wa kimasonia ili mjue ya kuwa televisheni ni haramu na kuinunua ni haramu na kuiuza ni haramu,na hili halitilii shaka mwenye ufahamu wa dini ya Allah si*****

  • Televisheni ndani yake kuna picha[za viumbe nyenye roho],na kuingiza picha nyumbani ni haramu.Na kutoka kwa Aisha~~~hakika mtume wa Allahﷺ aliona kitambaa juu yake kuna picha ukabadilika uso wake…….” Na ama televisheni hajatulazimisha kwayo isipokuwa sheitwani na majeshi yake na ulinzi ni kwa Allah kutokana naye.

  • Na haya yote yanaelekeza juu ya uharamu wa kuingiza picha majumbani na kuwa televisheni ni haramu isipokuwa ili ambayo imetenzwa nguvu kwayo na imelazimishwa na madhambi ni juu ya mwenye kulazimisha watu katika haramu.

  • Amesema mtumeﷺ ” Malaika hawaingi nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa wala picha”Ameipokea Bukhari na Muslim kutoka kwa Aisha.

  • Ndani ya televisheni kuna picha za wanawake,haijuzu kwa mwanaume kuwaangalia na picha za wanaume haijuzu kwa mwanamke kuwaangalia.

       Amesema Allah aliyetukuka “Na waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Allah anazo khabari za wanayoyafanya.[30] Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao…..”[An nuur 30-31]

       Na kama ilivyokuja kwa imamu Muslim Allah amrehemu kutoka kwa Jun-dubا amesema nilimuuliza mtume wa Allahﷺ kutokana na kuangalia[wanawake] kwa ghafla[bila kukusudia] akasema “geuza macho yako.”

Naapa kwa Allah juu yenu enyi waislamu,ni nani aliyeruhusu kwa mwanaume kumuangalia mwanamke aliyepigwa picha katika televisheni?na ni nani aliyeruhusu kwa mwanamke kuwaaangalia wanaume isipokuwa maadui wa Allah kwa kutumia hiki kifaa kichafu.

       Hili linatosheleza kuwa kifaa hicho ni haramu,uko wapi wivu wako ewe muislamu juu ya mke wako kuwaangalia wanaume tofauti na wewe? na uko wapi wivu kwa mwanamke juu ya mme wake?UMEONDOKA wala haula wala quwwata illa billah.

     Amesema Allah aliyetukuka “Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo “[An-nuur:63]

  • Televisheni inaharibu watoto na inadhuru dini yao na inawafungamanisha na asiyekuwa Allah na unawatumbukizia fikra za makafiri na inawarahisishia maasi na kujifananisha na makafiri

       Amesema Allah aliyetukuka“Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote[92]Kwa waliyo kuwa wakiyatenda”[93][suratun hijr 92-93]

Na amesema mtume wa Allahﷺ ” Kila mmoja wenu ni mchunga na kila mmoja wenu ni mwenye kuulizwa kutokana na uchunga wake,kiongozi ni mchunga na ni mwenye kuulizwa kutokana na uchunga wake, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumba yake na ni mwenye kuulizwa kutokana na uchunga wake na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mume wake na mwenye kuulizwa kutokana na uchunga wake,na mtumishi ni mchunga katika mali ya bwana wake na mwenye kuulizwa kutokana na uchunga wake,amesema Ibn Umar,na nadhani kuwa hakika amesema na mwanaume ni mchunga katika mali ya baba yake na mwenye kuulizwa kutokana na uchunga wake na nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ni mwenye kuulizwa kutokana na uchunga wake,”Kutoka kwa Ibn Umar katika sahihi mbili.

Na kutoka kwa kwa Ma’qil Ibn Yasar amesema,amesema mtume wa Allahﷺ ”Hamna mja yoyote Allah alimtawalisha raia kisha haku***kwa nasaha isipokuwa hakuipata harufu ya pepo”Ameipokea Bukhari na Muslim

amesema mwanachuoni Ibn Uthaymeen Allah amrehemu”Mwenye kufa na katika nyumba yake kuna kifaa hiki[king’amuzi]basi mtu huyo ni muongo kwa raia wake,inaogopewa juu yake……….”mpaka mwisho wa maneno yake Allah amrehemu.

  • Televisheni ndani yake kuna ubadhilifu wa mali.

Na amesema Allah aliyetukuka “wala usitumie ovyo kwa fujo” na amesema ﷺ ”Hakika watu wana*** katika mali ya Allah bila ya haki wana wao moto siku ya kiama”Ameipokea Bukhari kutoka kwa Khaulah~~~

Basi ni kutokea wapi na kwa haki ipi naapa kwa Allah juu yenu mnatoa mali katika kununua hivi vifaa na mnavipeleka kwa waislamu kwa mali nyingi?na vilievile kuviendesha kwa malil nyingi? Na kwa kila hela sisi ni wenye kuhesabiwa juu yake siku ya kiyama.

Na katika hadithi ya Abi Barzah amesemaﷺ ”Hautahama mguu wa mja yoyote siku ya kiyama mpaka aulizwe kutokana na umri wake ni katika lipi aliumalizia na kutokana na elimu yake ni katika lipi alifanya na kutokana na mali yake kutoka wapi aliichuma na wapi aliitoa na kutokana na mwili wake***”

  • Televisheni ni sababu ya kujifananisha na makafiri

amesema Allah aliyetukuka “Wala msiwe kama wale walio msahau allah, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao “[Al hashr 19]

Na kutoka kwa Abu Said Al khudriy amesema, amesema mtume wa Allah ﷺ ”Kwa hakika mtafuata njia za wale waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na dhiraa kwa dhiraa”Ameipokea Bukhari na Muslim

Na amesema mtume wa Allah ﷺ ”Mwenye kujifananisha na watu naye ni katika wao”Ameipokea Ahmad

Na mayahudi na manaswara wametutakia shari si kheri pale walipotutumia hii shari,utamuona muislamu ni mwenye kunyoa ndevu zake kwa sababu ya yale anayoyaona katika kifaa hiki na mtume wa Allah ﷺ amesema”Nendeni kinyume na washirikina punguzeni masharubu na achene ndevu”Ameipokea Muslim kutoka kwa Ibn Umar.

Utawaona wanavaa bantwaluni[suruali zenye kubana] kwa sababu ya yale wanayoyaona katika televisheni,na hii ni katika mavazi ya makafiri,na hivihivi[wanafanya] katika mengi ya matendo yao.TunamuombaAllah afya na salama.

  • Televisheni inamuingiza mtu katika bidaaNa amesema Mtume wa Allahﷺ ”Mfano wa swahiba mwema na swahiba muovu ni kama mfano wa mtengenezaji miski na mfuaji vyuma*** *** kutoka kwa mtengenezaji miski ima uinunue miski hiyo au upate harufu yake,na mfuaji vyuma ima aunguze mwili wako au ngozi yako au upate kutoka kwake harufu mbaya”Wanamuingiza muislamu katika bidaa zao na fikra zao chafu ambazo dini yetu iliyo twahara ya kumuabudu Allah na kutomshirikisha na yoyote haiziridhii.Na pia hadhihiri katika televisheni isipokuwa aliye miongoni mwa watu wa bidaa

  • Na amesema Ibn Siyriin”Hakika elimu hii ni dini basi angalieni kutoka kwa nani mnachukua dini yenu”Na hili na miongoni mwa yenye dhambi kubwa zaidi nalo ni kuwa baadhi yao wanatoa hoja kwa kutumia wale wanaoenekana katika televisheni miongoni mwa wanachuoni waovu katika stesheni za shari kama stesheni ya ALMAJD na stesheni ya IQRA .

  • amesema Allah aliyetukuka” Na wala msiwe katika washirikina.[31]Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho.”[32]   [Ar ruum 31-32]

  • Televisheni inaondosha tabia njema Na pia tusisahau ya kuwa televisheni inadhuru mwili kama macho na nyinginezo miongoni mwa neema ambazo ni wajibu juu yetu kumshukuru Allah kwazo,tusimuasi kwazo.

  • Na Allah amesema” Na hakika wewe una tabia tukufu“[Al qalam:4] na televisheni inaondosha tabia njema na inajalia sehemu ya tabia njema tabia chafu zilizoharamishwa.Inaondoa wivu kutoka kwa mwanaume na mwanamke na inaondoa haya na utukufu na ushujaa na kujizuia na heshima na nyinginezo katika sifa nzuri za kiislamu.Na huweka mahala pa sifa njema sifa mbaya miongoni mwa alizoziharamisha Allah,zingatieni enyi watu wenye uoni.

  • Katika televisheni kuna nyimbo amesema Ibn Masoud na kundi katika wema waliotangulia”Hakika mazungumzo ya upuuzi ni wimbo”Na wamesema baadhi ya watu wema “Hakika wimbo unaotesha unafiki katika moyo”Mapenzi ya kitabu na mapenzi ya sauti za wimbo         katika moyo wa mja yoyote hayakusanyiki

  • Na amesema Ibnil Qayyim;

  • Na amesema mtume wa Allahﷺ ”Watakuwa watu katika umma wangu wanahalalisha ***hariri na pombe na ***”Ameipokea Bukhari

  • Amesema Allah Aliyetukuka”Na miongoni mwa watu wapo wana nunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Allah pasipokujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha.“[luqman-6]

  • Televisheni hupelekea katika tabia mbaya na vifundo na talaka baina ya mke na mume.

  • Na haya ni katika adhabu za Allah kwa mwenye kuingiza kifaa hiki katika nyumba yake.Utamuona mtu ameghurika na wanawake wazuri na kuangalia katika nyuso***,inakinai nafsi yake kutokana na mke wake akawa hamuangalii wala hamjali na hivyohivyo mwanamke huweza kuona aliyekuwa mzuri kuliko mme wake kinguvu na uzuri wa uso akawa hamjali mumewe na yumkini likapelekea hilo katika kutengana wala *** kutoka kwa wawili hao.Na yameshatokea haya na Allah ndio mwenye kutakwa msaada

  • Televisheni inapelekea katika kukaa na watu wa uharibifuMche Allah ewe ambaye unawahalalishia watu kile alichokiharamisha Alah na wala huangalii katika madhara yake na uharibifu wake.Kwa hakika Allah ameharamisha pombe pamoja na yaliyopo ndani yake katika manufaa ambayo Allah ameyaita kuwa ni manufaa kwa sababu ya madhara yanayopatikana ndani yake ya **** nafsi na vifundo.Hamna budi kwa mwanadamu ajitahidi kwa ajili ya dini yake kuliko anavyojitahidi kwa ajili ya dunia yake,amtake fatwa yule ambaye anaona yuko pamoja na haki na yuko mbali na dunia na starehe zake na maslahi yake,na wale ambao wapo mbali na makundi ya kisiasa yanayotoka kwa makafiri.Na mwenye kutoa fatwa kinyume na hiyo[ya kuharamisha] basi hilo ni kosa lililo wazi na wewe pupia juu ya dini yako ****.NA KILA SIFA NJEMA ZINAMSTAHIKI ALLAH

  • Amesema Allah Aliyetukuka “Basi na watahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo “ [An-nuur:63]      

  • Tunamuomba Allah azitengeneze hali za waislamu na atuongoze katika haki.

  • Angalia katika fatawa za maimamu kama Ibn Baaz na Al-albaniy na Ibn Uthaymeen na shekhe wetu imamu Alwadiy rehma za Allah na msamaha wake uwe juu yao.Kwa hakika wametoa fatwa juu ya kuharamisha televisheni,na hili ndilo lililo maarufu katika vitabu vyao na fatawa zao kama si kuogopea kurefusha risala hii tungezitaja fatawa hizo.

  •      Na kwa hakika amesema Mtume wa Allahﷺ ”Lenye kuogopesha zaidi ninaloliogopea juu ya umma wangu ni wanachuonni wenye kupoteza “ na amesema “Uovu ni kilie kinachotia shaka katika nafsi yako na hata kama watu wakikutolea fatwa na wakakutolea fatwa.

  • Amesema mtumeﷺ ”Mfano wa swahiba mwema ….’’Naapa kwa Allah juu yako ewe muislamu je hiki kifaa ni swahiba muovu au swahiba mwema ?Hamna shaka ya kuwa jawabu la mkweli na mwenye kuelewa ya kuwa ni swahiba muovu na hata kama itapatikana kutoka katika televisheni yale wanayoyaona baadhi ya watu kuwa ni kheri na ni dini.Kwa kuwa madhara yake ni mengi zaidi na ***na uharibifu wake ni mkubwa na ***

 

أضف تعليقاً

لن يتم نشر عنوان بريدك الإلكتروني. الحقول الإلزامية مشار إليها بـ *

يمكنك استخدام هذه HTML الدلالات والميزات: