HUKUMU ZA SIKU KUMI [ZA MWANZO KATIKA MWEZI WA] DHUL-HIJJA.
بسم الله الرحمن الرحيم
HUKUMU ZA SIKU KUMI [ZA MWANZO KATIKA MWEZI WA] DHUL-HIJJA.
Kila sifa njema ni zake Allah mwenye kuhimidiwa na sala na salamu kwa mtume wetu na ahli zake na maswahaba wake na waliokuja baada yao, ama baada;
Hakika Allah ameweka kuwa ni sheria kwa waja wake yale yenye kuwanufaisha na amewakataza yale yenye kuwadhuru utakasifu ni wake Allah na ametukuka,amefanya hivyo kwa kuwaonea huruma.
Na hakika miongoni mwa aliyoyafanya kuwa ni sheria kwao na akawahimiza kwayo ni matendo mema katika kumi la kwanza [katika mwezi wa] Dhul-hijja(mfungo tatu).
Amepokea Imam Bukhari katika sahihi yake kutoka kwa Ibn Abbasا amesema mtume ض“hakuna katika siku matendo mema yanapendeza zaidi kwa Allah kuliko siku hizi(kumi la mwanzo katika Dhul-hijja), wakasema [maswahaba]”wala kupigana katika njia ya Allah?” Akasema mtume “[ndio] wala kupigana katika njia ya Allah,isipokuwa mtu aliyetoka kwa mali yake na nafsi yake na hakurejea na chochote katika hivyo.’’
Itumie fursa hii ewe mja wa Allah katika masiku haya kabla hayajakufika mauti, na haya ni masiku yenye kupita ambayo mwanadamu atakuta thawabu zake siku ya kiyama.
Na katika matendo mema katika siku hizi ni kukithirisha sala, swaum, sadaka, hajji, umra na kuchinja [kwa ajili ya Allah.]
HUKUMU YA KUFUNGA KATIKA MASIKU HAYA
Ama siku ya kumi ni haramu kufunga katika siku hiyo kwa kuwa ni siku ya idd. Ama siku ya tisa[siku ya ‘arafa] inapendeza kufunga katika siku hiyo nayo ni sunna iliyotiliwa mkazo.
Funga siku ya ‘arafa inafuta madhambi ya mwaka uliopita na mwaka uliopo kama ilivyothibiti kutoka kwa Abu Qatadaاkatika sahihi Muslim.
Ama siku zilizobakia imethibiti kwamba mtume ض hakufunga na kwa hakika alifunga siku ya ‘arafa na alikuwa anafunga siku ya jumatatu na alhamisi, na atakaefunga masiku hayo,hilo ni katika matendo mema,na atakaeacha akala hakuna ubaya.
NA KATIKA HUKUMU ZA KUCHINJA
-
Tambua hakika kuchinja sio wajibu na hii ni kauli ya jamhuri ya wanachuoni kinyume na Abuu Hanifa,Imam Awza’ii na wengineo.
-
Na inakuwa wajibu kwa yule anaetaka kuchinja yanapoingia masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-hijja kutonyoa nywele zake wala kukata kucha zake,Ameipokea imam Muslim kutoka kwa Ummu Salama.Kumesemwa hekima inayopatikana katika jambo hili, ni kujifananisha na mahujaji.Na kumesemwa ni ili abaki[mchinjaji]] na viungo vyake vyote vya mwili. Na jambo hili ni la kiibada.
-
Na hii hadithi ni dalili ya kukosekana uwajibu wa kuchinja, kinyume na Abu Hanifa.
-
Inapendeza kuchinja mnyama aliyenenepa na mzuri na kwa kuwa hili ni katika kutukuza alama za Allah, kwa hadith ya Abu Umamah bin Sahliاamesema”Tulikua katika mji wa madina tunanenepesha vichinjwa, na walikua waislamu wananenepesha[vichinjwa]”. Imepokewa na Bukhari
-
Na imeshurutishwa kuwa MUSINNA(mnyama aliyeng’oka meno ya mbele kisha yakaota mengine), kwa hadithi ya Jabirاamesema,amesema mtumeض’’Msichinje isipokuwa MUSINNA,ila itakapowawia ugumu chinjeni JADHA’A katika kondoo.’’ Imepokewa na Muslim Na JADHA’A katika kondoo ni mwenye mwaka mmoja kamili,na imesemwa tofauti na hivyo. Na kile kichopokelewa kuhusu mnyama aliyevunjika pembe na kasoro katika masikio kuwa hawafai, haijathibiti dalili na pia yule aliyekatwa makalio. Na uhalisia ni kuwa inaruhusiwa kuchinja mfano wa wanyama hawa, na akipatikana aliyesalimika kutokana na haya ni bora.
-
Na inashurutishwa kwa vichinjwa kutokuwa na kasoro na usahihi uliokuja katika mlango huu ni hadith ya Baraa bin Aazibاamesema; amesema mtum ض’’Vitu vinne havifai katika vichinjwa, chongo uliobainika uchongo wake,mgonjwa uliobainika ugonjwa wake, kilema uliobainika ukilema wake na mkubwa ambaye hana uroto katika mifupa yake[amezeeka].’’Ameipokea Abu Daud, Tirmidhi na Nasaai na ni sahihi, na katika hili wamewafikiana wanachuoni.
-
Wamesema wanachuoni,MUSINNA ni kila mnyama aliyeota meno ya mbele katika ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo.
-
Inajuzu kuchinja mbuzi mmoja kwa watu wa nyumba moja kwa hadith ya Abu Ayubuا’’Alikuwa mtu katika zama za mtume ض anachinja mbuzi mmoja kwa ajili yake na watu wa nyumbani kwake’’Ameipokea Ibn Maja.
-
Na hakuna budi kusema bismillaah, amesema Allah’’Na wala msile katika vile[vichinjo] ambavyo halikutajwa juu yake jina la Allah. [Kwani] huo ni uovu.’’ [al anaam 121]
-
Na anazidisha baada ya kusema bismillah kusema ALLAHU AKBAR katika vichinjo vya masiku hayo.Kutoka katika hadith ya Anas ا.
-
Na inapendeza kwa imam kuchinja uwanjani kwa hadith ya Ibn Umarا’’hakika mtume ضalikuwa anachinjia uwanjani’’Ameipokea imamu Bukhari.
-
Kumesemwa hekima yake ni walione hilo masikini na wapate katika kichinjwa hicho.
-
Ama wakati wake ni baada ya swala ya idd kwa kauli iliyokuwa sahihi,mpaka mwisho wa masiku ya tashriiq(siku tatu baada ya siku ya idd) kwa hadith ya Anasاamesema; amesema mtumeض’’yule atakaechinja kabla ya swala[ya iddi] arudie kuchinja [baada ya swala]. Ameipokea Bukhari na Muslim.Na kutoa sadaka kwa masikini kama alivyosema Allah’’Na mlisheni mwenye shida aliye fakiri’’[surat hajj 28] ALLAH ATUKUBALIE SISI NA NYIE MATENDO YETU NA KAULI ZETU.
-
-
Na inafaa kutunza atakavyo katika kichinjo hicho kwa sababu makatazo ya kutunza yamefutwa.
-
Na inapendeza ale sehemu katika kichinjo hicho kwa kauli ya Allah ‘’Basi kuleni katika hao’’ [surat hajj 28]
مرتبط