«

»

Kila sifa njema ni zake Allah na swala na salamu ziwe juu ya mtume ﷺ, anasema Allah, (basi wakiamini kama vile mlivyoamini nyinyi{maswahaba} basi watakuwa wameongoka).

بسم الله الرحمن الرحيم

Kila sifa njema ni zake Allah na swala na salamu ziwe juu ya mtume ﷺ, anasema Allah, (basi wakiamini kama vile mlivyoamini nyinyi{maswahaba} basi watakuwa wameongoka).

Hakika katika sunna zilizohamwa ni kunyosha safu katika swala.

Na watu wengi hawajali jambo hilo la kunyosha safu na wanadhania kuwa wameongoka.

Na ajue kila muislamu kwamba kutofautiana katika safu ni miongoni mwa sababu za kutofautiana hakika na kutofautiana nyuso na nyoyo, amepokea imam Bukhari kutoka kwa Nuuman bain Bashir — anasema, amesema mtume ===, “mtanyoosha safu zenu au atatofautisha Allah baina ya nyuso zenu”.

Na amepokea imam Muslim kutoka kwa abuu Masuud — amesema, alikuwa mtume === anagusa mabega yetu katika swala huku akisema “nyosheni safu, na wala msikhitilafiane mkatufautishwa mioyo yenu, wanifuate mimi nyuma yangu wenye akili na uerevu kisha wale wanaowafuata kisha wale wanaowafuata”. Akasema abuu Masuud, “hakika nyinyi leo hii mnakhitilafiana sana.”

Na kunyosha safu ni katika kuifanya swala kuwa nzuri na kuitimiza, amepokea Bukhari kutoka kwa abuu Huraira — kutoka kwa mtume === kua anasema, “hakika amewekwa imamu ili afuatwe, …. na nyosheni safu katika swala hakika kunyosha safu ni katika uzuri wa swala”. Ameipokea Muslim

Allah anaamrisha katika kitabu chake katika sehemu kumi na sita(16) kuhusu kusimamisha swala, (simamisheni swala na mtoe zaka) muzamil 20. Na katika kusimamisha swala ni kunyosha safu amepokea Bukhari kutoka kwa Anas bin Malik — kutoka kwa mtume === amesema, “nyosheni safu zenu hakika kunyosha safu ni katika kusimamisha swala”. Ameipokea muslim

Na kutimiza safu nimkatika sifa za malaika katika safu zao mbele ya mola wao amepokea imam Muslim kutoka kwa Jabir bin Samura — amesema, alitoka kwetu sisi mtume === akasema, “hivi msinyoshe safu kama wanavyonyosha malaika mbele ya mola wao?” tukasema, “ewe mtume wa Allah, vipi wanyosha malaika safu mbele ya mola wao?” akasema, “wanatimiza safu ya kwanza na wanayoka katika safu zao”.

Na amepokea Muslim kutoka kwa Anas bin Malik — amesema; amesema mtume wa Allah ===, “nyosheni safu zenu, hakika kunyosha safu ni katika kutimiza swala”.

Na alikuwa mtume === akisubiri mpaka zinyoshwe safu, imepokewa kutoka kwa Nuuman bin Bashir — anasema, “alikuwa mtume === akinyosha safu zetu kana kwamba ananyosha msale mpaka aone tumeshafahamu, kisha akatoka siku moja mpaka akakaribia kuleta takbira ya kuanza swala akaona mtu kifua chake kimetokeza kwenye safu, akasema, “enyi waja wa Allah mtanyoosha safu zenu au atatofautisha Allah baina ya nyuso zenu”.

Na katika sunna ni kulinganisha safu, amepokea Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira amesema, “ilisimamishwa swala na zikalinganishwa safu sawasawa, akatoka mtume ===.

Na katika sunna ni watu kupanga safu kwa kusaidiana na imam, amepokea imam Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira — amesema, “kulikimiwa swala wakanyosha watu safu zao, akatoka mtume === akatangulia kwa ajili ya kuswalisha, hali ya kuwa ana janaba, kisha akasema, “lazimianeni na sehemu zenu” kisha akarudi akaoga, kisha akatoka na kichwa chake kina nyunyuzika maji, akatuswalisha”.

Na walikuwa maswahaba wanaifanyia hima sunna hii, imethibiti kutoka kwa Anas bin Malik — hakika yeye alifika Madina akaambiwa; haujawahi kutukataza sisi tokea siku ambayo ume ……………………….? akasema, “…………………… isipokuwa nyinyi hamnyoshi safu”. Ameipokea Bukhari.

Na amepokea AbdurRazaak hakika Ibn Umar — alikuwa akisema: “ katika kutimia swala ni kunyosha safu”. Sanad yake ni nzuri. Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Umar — amesema, “alikuwa Umar apigi takbira ya kuhirimia swala mpaka zinyoshwe safu, anawakilisha katika kunyosha safu baadhi watu”.

ZILE ZILIZOTHIBITI KUTOKA KWA MTUME === KATIKA ADHKARI ZA KUNYOSHA SAFU.

1.        Nyosheni safu zenu kwa hakika kunyosha safu ni katika kusimamisha swala Ameipoka Bukhar kutoka kwa Anas kutoka kwa mutume*****

Na ameipokea Musilim kutoka kwa Anas kwa lafudhi ‘ nyosheni safu zenu hakika kunyosha safu ni katika utimilifu wa swala

  1. Kwa hakika mtazinyosha safu zenu au atatofautisha Allah baina ya nyuso zenu Ameipoka Bukhar kutoka kwa Nuuman ibn Bashiir

  2. Enyi waja wa Allah mtazinyosha safu zenu au Allah atatofautisha baina ya nyuso zenu Ameipokea Musilim kutoka kwa Nuuman Inb Bashiir

  3. Nyosheni safu nyosheni safu nyosheni safu Ameipokea Annasaay kutoka kwa Anasi kuwa mtume *****         alikuwa akisema ‘Nyosheni safu nyosheni safu nyosheni safu Amesema shekhe albaan hii hadiithi ni sahihi

  4. Wekeni sawa baina ya mabega na zibeni mianya na kuweni wa laini katika mikono ya ndugu zenu na wala msimwachie shaitwani upenyo na mwenye kuunganisha safu Allah atamuunganisha na mwenye kuikata safu Allah atamkata Ameipokea Ahamadi kutoka kwa Abdullah Ibn Amur kutoka kutoka kwa mtume *****         na isinadi yake ni nzuri

  5. Nyosheni safu na wala msitofautiana zikatofautia nyoyo zenu wanifate nyuma yangu katika nyinyi wenye akikili na uelevu kisha wanao wafuata kisha wanao wafuata Ameipokea     Muslimu kutoka kwa Ibn Masuud na kaipokea Ahamad kutoka kwa Anuuman Ibn Bashiir

  6. Wanifuate nyuma yangu katika nyinyi wenye akili na uelevu kisha wale wanao wafuata [mara tatu] na chukuweni tahadhari kutoka na masauti ya masokoni Ameipokea musilim [432] kutoka kwa Abdullah Ibn Masuud

  7. Ziwekeni sawa safu zenu na zikaribisheni baina yake nazilinga nisheni shingo Ameipokea Abuu daudi[667] kutoka kwa Anasi Ibn Maliki sanadi yake ni sahihi amesema shekhe aliban hadithi hii ni sahihi Tunamuomba Allah mtukufu   awaafikishe waisilamu kuzisimamisha swala zao na kuzifanya vizuri safu zake na awaafikishe kufanyia kazi sunna na kuwafuata wema walio tangulia na Allah ndiye mwenyekutakwa msaada utakasifu ni wake

  8. Na haijuzu kwa imamu kusema yale matamko ambayo yamezushwa matamuko ambayo hakuyasema mutume ***** mfano ;[hakika ya Allah haiangalii safu iliyo pinda] au[jiangalieni] au matamko mengineyo yasiyo kuwa haya katika yale ambayo haya kutiwa sheria na sunna kutoka na haya matamko ni yenye kujitosheleza

أضف تعليقاً

لن يتم نشر عنوان بريدك الإلكتروني. الحقول الإلزامية مشار إليها بـ *

يمكنك استخدام هذه HTML الدلالات والميزات: