(Ewe mola wetu mlezi, tupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe ni waongozi kwa wamchao Allah.) Alfurqaan 74.
Kila sifa njema ni za Allah ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu na akaanzisha kumuuba mtu kwa udongo, na ninashuhudia ya kwamba hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah hali ya kuwa yuko peke yake hana mshirika, shahada ya haki ninatarajia manufaa yake siku ya malipo, ama baada; na swala na salamu ziwe juu ya mtume wake === na ziwe juu ya watu wake na maswahaba zake,
Amesema Allah katika kitabu chake, (na katika alama zake ni kuwa amekuumbieni wanawake kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, na akajaalia mapenzi na huruma baina yenu.)
Na imethibiti katika hadithi iliyopokelewa na aisha ~~~, “Oeni wanawake wenye mapenzi wenye kuzaa, kwa sababu mimi ni mwenye kujikithirisha kwa wingi wa watu mbele ya manabii siku ya kiama”. Ameipokea Ahmad
Kwa hakika mwenye kuoa na akataka kumuingilia mkewe, kuna adabu za kiislam ambazo wengi wamechanganyikiwa au hawazijui. Chukua adabu hizo;
BAADHI YA ADABU ZA NDOA ZA KUINGIA NDANI.
1-Inambidi aseme yale yaliyokuja katika kauli yake mtume === pindi atakapooa mmoja wenu mwanamke au kumnunua mtumwa amshike utosini mwake na aseme (BISMILLAH) na ombe baraka na aseme, “ewe Allah ninakuomba kheri zake na kheri uliyomuumbia juu yake na unikinge na shari zake na shari ulizomuumbia juu yake”. Ameipokea Bukhari katika AF’AAL IBAAD
2-Na inapendeza kwa wanandoa wawili kuswali pamoja rakaa mbili kwa sababu jambo hili limenukuliwa kutoka kwa wema waliotangulia, Imepokelewa kutoka kwa Abdillah bin Mas’uudi — kwamba yeye amesema, “Pindi atakapoingia mwanamke kwa mumewe, mwanamume asimame na mwanamke asimame nyuma yake waswali pamoja rakaa mbili”. Ameisahihisha imam Albany
3-Kumfanyia upole mwanamke wakati wa kukutana naye;
Inapendeza kwa mwanamume pindi atakapoingia kwa mke wake amfanyie upole kama vile kumtangulizia sehemu katika kinywaji na kinginecho kutokana na hadiithi ya Asmaa bint Yaziida ~~~ amesema, “nilimpamba Aisha kwa ajili ya mtume === kisha nikamuita aje kumfunua na kumwangalia, alikuja akakaa pembezoni mwake akaletewa chombo kikubwa cha maziwa akanywa kisha akampatia Aisha”.
4-Inambidi aseme wakati anapotaka kumuingilia mkewe (BISMILLAH, ewe Allah tuepushe na shetani na umuweke mbali shetani na kile utakacho turuzuku, ikiwa Allah atakadiria baina yao mtoto hatodhuriwa na shetani milele). Imepokewa na bukhari na muslim
5-Asimuingilie mkewe katika utupu wa nyuma wala akiwa katika hedhi (siku zake).
Anasema Allah, (basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi). Na amesema mtume ===, “Allah hatomuangalia mtu ambaye anamuingilia mkewe katika utupu wa nyuma”.
6-Yanayomuhalalikia wakati wa hedhi;
Inajuzu kwa mwanaume kustareheka na mke wake ispokuwa katika utupu wake kutokana na hedhi na katika hili kuna hadithi ya mtume === inakataza “fanyeni kila kitu ispokuwa tendo la ndoa”. ameipokea muslim kutoka kwa Anasi —.
7-Kutawadha baina ya jimai mbili (tendo la ndoa).
Pindi atakapomuingilia mkewe katika ile sehemu iliyoruhusiwa kisheria kisha akataka kurejea tena sehemu hiyo atawadhe kutokana na kauli ya mtume ===, “pindi mmoja wenu atakapo muingilia mke wake kisha akataka kurudia basi atawadhe baina ya jimai mbili (tendo la ndoa). Na imekuja katika mapokezi mengine “atawadhe kama anavyotawadha kwa ajili ya kuswali, kwa sababu kufanya hivyo kunamtia uchangamfu wa kurudia (tendo la ndoa)”. Ameipokea Muslim kutoka kwa Abuu Said —
8-Inajuzu kwa wanandoa wawili kuoga pamoja na hata kama wataonana
Imepokewa hadithi kutoka kwa Aisha ~~~ kwamba amesema, “nilikuwa nikioga mimi pamoja na mtume === katika chombo kimoja kilichopo baina yangu mimi na yeye kiasi kwamba mikono yetu ilikuwa ikipishana katika chombo hicho alikuwa akishindana na mimi hadi nikasema nibakizie nibakizie” akasema Aisha ~~~ tulikua katika hali ya janaba. Ameipokea Bukhari na Muslim
9-wasilale hali ya kuwa wana janaba, ispokuwa watakapotawadha
Imepokewa hadithi kutoka kwa aisha ~~~ kuwa amesema, “alikuwa mtume === pindi anapotaka kula au kulala na hali ya kuwa ana janaba anosha utupu wake, na anatawadha udhu wa swala”. Ameipokea Bikhari na Muslim. Na imepokelewa hadithi kutoka kwa ammaar bin yaasir — kwamba mtume === amesema, “watu wa sampuli tatu malaika hawa wakaribii, maiti ya kafiri, mwanaume anaejitia manukato ya kike na mwenye janaba ispokuwa atakapooga). Ameipokea Bayhakii.
10-ni wajibu kwa mwanaume kuishi naye kwa wema na kumfanyia wepesi katika kile alichohalalishiwa na sio katika kile alichoharamishiwa na hasahasa atakapokuwa ni msichana wa umri mdogo; kutokana na kauli yake mtume ===, “mbora wenu ni yule ambaye ni mbora katika ahli zake na mimi ni mbora wenu kwa ahli zangu”. Ameipokea Tirmidhi.
11-inatakikana kwao wanuie kwa ndoa yao kuzihifadhi nafsi zao na kuzichunga ili wasiingie katika yale aliyowaharamishia Allah kwa sababu kile kitendo chao cha ndoa ni swadaqa, Kama ilivyokuja hadithi ya Abii Dhari — kuwa amesema mtume ===, “na katika tendo la ndoa la mmoja wenu ni sadaka” maswahaba wakasema ewe mtume wa Allah, je, kuna thawabu ikiwa mmoja wetu atajitosheleza matamanio yake kwa kufanya tendo la ndoa? Akasema mtume ===, “je, hamuoni kwamba ikiwa atajitosheleza kwa yaliyo ya haramu si ingelikuwa ni dhambi juu yake?” Wakasema ndio akasema mtume ===, “hivyohivyo akikidhi matamanio yake katika halali anapata ujira”.
12-uwajibu wa walima (karamu ya harusi)
Hapana budi kwake yeye kufanya walima baada ya kumuingilia mkewe kama alivyomwamrisha mtume === Abdurahmaan bin Awfu — kama ilivyokuja katika hadithi ya Anas — kuwa amesema mtume ===, “Allah akubariki; fanya walima (karamu) japo wa mbuzi mmoja”. hakalijuzisha hilo. Ameipokea Bukhari
13-kuitikia mwaliko.
Inambidi kuitia mwaliko na hata kama atakuwa yupo katika swaumu kwa kauli ya mtume ===, “pindi atakapoitwa mmoja wenu katika chakula basi na aitikie mwito, ikiwa hakufunga basi ale na ikiwa ni mwenye kufunga basi amuombee dua (mwalikaji)”. Ameipokea Muslim kutoka kwa Abuu Huraira.
14-kutokuitikia mwaliko ambao ndani yake kuna maasi, isipokuwa akiwa amekusudia kuyakemea na kujaribu kuyaondoa na kama sio hivyo ni wajibu kwake kurejea. Imepokelewa kutoka kwa Ali — kuwa amesema, “niliandaa chakula kisha nikamuita mtume === akaja akaona picha nyumbani, akarejea” akasema Ali — nikasema kumuuliza mtume === “ewe mtume wa Allah ni kitu gani kimekurejesha? Akasema mtume === “kwa hakika kwenye nyumba kuna pazia lenye picha na kwa hakika malaika hawaiingii nyumba yoyote ambayo ina picha”. Amesema al-imaam al-awzaiy, “hatuingii katika walima(chakula cha harusi) ambao kuna ngoma na firimbi”. Ameisahihisha imam Albany
15-kumuombea dua ya kheri na baraka yeye na mke wake; imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin Abdillah — amesema kuwa mtume === amesema, “Allah akubariki”. Ameipokea Bukhari na Muslim. Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira — kwamba mtume === alikuwa akimpongeza mtu pindi anapooa, anasema, “Allah akubariki na abariki juu yako na awakutanishe baina yenu katika (na imekuja katika riwaya; juu) ya kheri”. Ameipokea Addaramiy na Ahmad na ameisahihisha imam wadiiy.
16-nyimbo nzuri zisizokua na uovu na kupiga dufu.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha ~~~ kuwa alimsindikiza mwanamke mmoja kwenda kwa mumewe wa kianswari akasema mtume ===, “ewe Aisha hamkuwa na nyimbo zozote (mlipokuwa mkimsindikiza) kwani maanswari wanapenda viburudisho”. Ameipokea Bukhari na Haakim
MIONGONI MWA MAOVU KATIKA NDOA
amesema al-allaamatu al-albaaniyrahimahullahu; ni wajibu kwake yeye kujizuia na kila jambo ambalo linakwenda kinyume na sheria na hasahasa mambo ambayo watu wameyazoea katika mfano wa mnasaba huu (mnasaba wa ndoa) mpaka wakadhania wengi kwa sababu ya kunyamaza maulamaa kuwa hakuna tatizo (kuyafanya yalio kinyume na sheria)
na mimi ninatanabisha hapa juu ya mambo muhimu miongoni mwa hiyo;
(1)kutundika picha ukutani ni sawa picha hiyo iwe ni ya kiwiliwili au sio ya kiwiliwili au ina kivuli au haina kivuli imechorwa kwa mkono au kwa fotogorafia kwa sababu yote hayo hayajuzu na niwajibu kwa mwenye kuweza kuziondoa ikiwa hakuweza kuzichana.
Imepokelewa kutoka kwa aisha kuwa amesema (aliingia kwangu mtume hali ya kuwa nimefunika chumba cha hazina kwa pazia ambalo lilikuwa na picha ;
Na katika riwaya nyingine (ambalo lilikuwa lina picha za farasi wenye mbawa) mtume alipoliona alilichana na uso wake ukabadilika kuwa mwekundu
Na akaseme ;(ewea aishawatu watakao pewa adhabu kali kabisa mbele ya allah siku qiama ni wale wanaoingiza uumbaji wa allah;
Na katika riwaya (hakika wenye picha hizi wataadhibiwa na wataambiwa viwekeeni uhai mlivyoviumba) kisha akasema mtume (kwa hakika malaika hawaingii nyumba ambayo ina picha)
(2)kujifananisha na wanaume;chukua mambo yafuatayo;
(A)mwanamke kupunguza nywele kama mwanaume
(B)kuvaa bantwaloon (surual jinzi kadeli)
(C)kufanya tamthilia
(3)kuzipaka rangi kucha na kuzirefusha
Hii ada chafu imekuja kutoka kwa wanawake waovu kutoka nchi za uingereza na kuwafikia wanawake wa kiislam
Amesema mtume (mambo matano ni katika maumbile;kutairi,kunyoa nywele za sehemu za siri na kupunguza masharubu na kukata kucha na kunyoa nywele za kwapani)
Amesema anas radhwiyallahu anha ametuwekea muda mtume wa kupunguza masharubu na kukuata kucha kunyoa nywele za kwapani na kunyoa nywele za sehemu za siri kwamba tusiviache vitu hivi zaidi ya siku arobaini)
(4)kunyoa ndevu
Miongoni mwa vitu walivyopewa mitihani zaidi wanaume katika kupambiwa ni unyoaji wa ndevu kwa sababu ya hukumu yao ya kuwaiga makafiri wa nchi za uingereza mpaka ikafikia kuwa ni aibu kwa bwana harusi kuingia kwa bibi harusi hali ya kuwa hakunyoa ndevu.
Na katika hili kuna tahadhari nyingi;
(a) kubadilisha maumbile ya allah; na kwa hakika mtume amewalaani wale wanaobadilisha maumbile ya allah kwa ajili ya kutafuta uzuri.
Hakuna shaka kuwa ukataji wa ndevu kwa ajili ya kutafuta uzuri kunaingia katika laana.
(b)kwenda kinyume na amri ya mtume nayo nikauli yake (punguzeni masharubu na ziacheni ndevu).
((mtume wanaume wanaojifananisha na wanawake na wanawake wanaojifananisha na wanaume)).
Na wala haifichikani kwa mwanaume anayekata ndevu zake ambazo Allah amemtofautisha kwa ndevu hizo na mwanamke kuwa ndilo jambo kubwa ambalo ujifananisha na mwanamke;
Huenda kutokana na dalili ambazo tumezitaja ikiwa nisababu ya kukinaika na dalili hizo wengi waliopewa mtihani huu wa kwenda kinyume na ufugaji wa ndevu;
Tunamuomba allah atusamehe pamoja na wao katika kila jambo ambalo allah halipendi na kuliridhia.
(e)kunyoa nyusi.na hili ni katika kubadilisha maumbile ya allah
Imepokelewa kutoka kwa ibn mas-uud kwamba mtume (amewalaani wanawake wanao jichora tatloo(kujichanja na kuweka alama katika mwili)
Na wanaoomba kuchorwa tatloo na wanaonyoa nyusi na wanaoweka mianya katika meno ili kutafuta uzuri na wanaobadilisha maumbile ya Allah mtukufu)
(5)pete ya uchumba
Uvaaji wa baadhi ya wanaume pete ya uchumba ambayo wanaiita pete ya uchumba ili pamoja na kuwa kuwaiga makafiri hivyohivyo jambo hilini katika ada zitokazo kwa wakristo.
Nyimbo ni haramu kwa kauli ya Allah
(ni miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi ili wawapoteze watu na njia ya Allah pasipokujua na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha)
Amesema IBN MAS-UUD na wengineyo katika maswahaba namuapia ALLAH maneno ya upuuzi katika aya hii ni nyimbo
Na kauli yake mtume (watakuwapo watu katika umma wangu watahalalisha……………
inatosha kuwa ni haramu kama walivyo sema maswahaba na mataabina kuwa nyimbo ni sauti za shetani;
-Na wamesema baadhi ya salafi;nyimbo ni miongoni mwa sauti ovu na zimelaaniwa.
-Na wamesema baadhi ya salafi; nyimbo ni sababu inayopumbaza kuacha kutomtaja ALLAH na inapelekea kupoteza katika ALLAH.
-Na wanasema baadhi ya salafi (wema waliotangulia)nyimbo ni miongoni mwa uzushi;
-Na wanasema baadhi ya salafi;
Nyimbo ni miongoni mwa midundo ya kibatili na nyimbo za ngoma ni katika ………….?
-mambo ya kijaabilia ambayo ALLAH ameyasema vibaya na kuyakemea.
-Na wamesema baadhi ya salafi nyimbo ni kaika mghafiliko upuuzi
Amesema ALLAH (nanyi mmeghafilika kuimba)
-wamesema baadhi ya salafi;
nyimbo ni midundo ni mjumbe wa ZINAA na mchochezi wa matamanio ya uovu.
Imepokewa kutoka kwa FUDHWEYL BIN IYAADH kuwa yeye amesema nyimbo ni ruqia ya uzinifu.
-Na wamesema baadhi ya salafi;
nyimbo ni zinaa ya masikio
-Na wamesema baadhi ya salafi;
(Nyimbo zinapelekea kuwa na matamanio ya kupenda taswiira ) picha na kupamba uchafu (zinaa).
-Na wamesema baadhi ya salafi;
Kudumu katika miziki na nyimbo kunaifanya QUR’AAN kuwa nzito katika moyo.
-Na wamesema baadhi ya salafi;
Nyimbo …………ni alama ya mnywa pombe
-Na wamesema baadhi ya salafi;
Nyimbo zinarithisha udayyuuthi(mtu kutokuwa na wivu na mke wake)
-Na wamesema baadhi ya salafi;
Muziki na nymbo zinazuia usomaji wa QUR’AAN na zinasababisha hasira za ALLAH mwingi wa rehma.
-Na wamesema baadhi ya salafi;
Kujishughulisha zana za muziki na ngoma ni sababu ya uislam kusalitiwa na maadui.
(7)WANAWAKE KUJIPAKAA MANUKATO:
Kwa kauli yake mtume (mwanamke yeyote yule atakaejipakaa manukato akapita mbele za watu ili wapate kusikia harufu yake huyo anahesabiwa kuwa ni mzinifu)
(8)MAVAZI YANAYOMFANYA KUWA UCHI.
Imepokelewa hadithi kutoka kwa ABII HURAIRA kuwa amesema mtume (sampuli mbili za watu wa motoni sijawaona watu ambao wananijeledi kama mikia ya ng’ombe wanawapiga watu kwa mijeledi hiyo na wanawake ambao dhahiri wamevaa lakini wako uchi (wanavaa nguo nyepesi ambazo zinaonyesha miili yao)
Wenye kuinamisha mabega yao, wenye kutembea kwa maringo vichwa vyao kama vile nundu za ngamia zilizo pinda, wanawake hawa hawatoingia peponi na wala hawatapata harufu yake,na harufu yake inapatikana masafa kadha wa kadha)
Na vazi la umashuhuri amesema mtume (atakaevaa vazi la kimashuhuri hapa duniani ALLAH atamvalishavazi la udhalili siku ya QIYAAMAH).
(9)kufanya israfu katika kadi za mwaliko na ndani yake kunakujifananisha na makafiri.
(10)MAHARI KUWA GHALI.
Na hakika hili kuna uovu mwingi na uchache wa baraka,na kuwatilia ngumu masikini kutokuoa na ueneaji wa zinaa (kwa sababu ya mahari kuwa ghali).
(11)UBADHIRIFU NA ISRAFU KATIKA MAVAZI NA VYAKULA.
Amesema ALLAH (na wala msifanye ubadhirifu kwa hakika wabadhirifu ni ndugu wa mashetani na shetani ni mwenye kumkufuru mola wake mlezi.
NA MWISHO NINAWAUSIA WANANDOA WAWILI KUMTII ALLAH NA KUFUATA HUKUMU ZA DINI YAKE ZILIZO THIBITI KATIKA KITABU NA SUNNA.
NA JAMBO LA PILI KILA MMOJA KATIKA WAO ALIZIMIANE KWA KUSIMAMA
KILE AMBACHO ALLAH RADHISHA JUU YAKE KATIKA MAMBO YA WAJIBU NA HAKI ZA MWENZAKE NA WALA MWANAMKE ASITAKE KUWA SAWA NA MWANAUME KATIKA HAKI ZOTE NA WALA MWANAUME ASIJISHUGHULISHE NA KILE AMBACHO ALLAH AMEMFADHILISHA JUU YA MWANAMKE KATIKA UBWANA.
Mwisho angalia maneno ya SHEIKHL-ALBAAN katika kitabu chake AADAABU AZ-ZAFAAF na katika baadhi ya risala za ahlissunah!!!.