MISINGI SITA MIKUBWA
MISINGI SITA MIKUBWA
Miongoni mwa maajabu makubwa na alama kubwa zenye kujulisha kudra za mfalme mwenye kushinda(Allah). Misingi sita ambayo ameibainisha Allah ubainifu uliyokuwa wazi kwa wale wasio na elimu kuliko vile wanavyo dhania wenye kudhani, kisha baada ya ubainifu huo wameteleza wengi katika wale wenye kudai akili(uerevu) isipokuwa wachache wao.
Msingi wa kwanza. Kupwekesha dini kwa Allah pekee hana mshirika yeye, na kubainisha kinyume chake ambacho ni kumshirikisha Allah, na kuwa ayah nyingi katika Qur’an zinabainisha msingi huu kwa njia nyingi tofauti tofauti kwa kutumia maneno ambayo yanayo fahamika kwa yule ambaye ni mgumu kuelewa, kisha baada ya kutokea katika umma huu yale yaliyotokea, akawadhihirishia Sheitwan ikhlasw katika sura ya kuwapunguzia heshima watu wema na kuwa shusha katika hali zao, na akawadhihirishia wao kumshirikisha Allah ni kuwapenda watu wema na wafuasi wao.
Msingi wa pili. Ameamrisha Allah kushikamana katika dini na amekataza kufarikiana watu katika dini, akabainisha Allah jambo hili ubainifu uliyo wazi wanaufahamu ubainifu huu watu wasio na elimu(awaam), na akatukataza sisi tusiwe kama wale waliyo farikiana katika dini na waka ikhtalifiana kabla yetu wakaangamia, na akataja Allah ya kwamba ameamrisha waislamu kushikamana katika dini na amewakataza kufarikiana katikadini, na inazidisha uwazi wa jambo hili yale yaliyopatikana katika hadith za mtumeص katika ajabu ya maajabu katika jambo hili, kisha likajeuka jambo nakua kwamba kutofautiana katika misingi ya dini na matawi yake ndio elimu na fikh katika dini, na ikajeuka kwamba kulingania watu kushikamana katika dini halinganii jambo hilo isipokuwa ni mnafiki au mwendawazimu!!
Msingi wa tatu. Hakika katika ukamilifu wa kushikamana: ni kusikia na kutwii kwa yule aliye wekwa amiri juu yetu(mtawala) hata kama atakuwa(mtawala huyo) ni kijakazi wa kihabesh, akabainisha Allah jambo hili ubainifu uliyowazi wenye kutosheleza kwa njia nyingi miongoni mwa aina ya ubainifu kisheria na *****, kisha ikawa kwamba msingi huu hautambuliki kwa wale wengi wanaodai kua wana elimu, basi vipi wataufanyia kazi?!
Msingi wa nne. Kubainisha elimu na maulamaa na fiqh na wanazuoni, na kubainisha wale wenye kujifananisha nao hali ya kuwa hawafanani nao, na hakika amebainisha Allah misingi huu mwanzoni mwa Suratul Baqara katika kauli yake, {Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni, na timizeni ahadi yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu,…} [2:40] mpaka katika kuali yake {Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni zile neema zangu nilizo kuneemesheni, na nimewafadhilisha kuliko wengine wote.} [2:47]
Na inazidishwa uwazi kwa yale yaliyowekwa wazi na sunna(hadith) katika maneno haya mengi yaliyobainishwa ambayo yapo wazi kwa yule asiye na elimu ****, kisha likawa jambo hili ni geni mno, na ikawa elimu na fiqh ndio bidaa na upotevu, na jambo bora walilokuwa nalo ni kuivalisha haki batili, na ikawa elimu ambayo Allah ameifaradhisha kwa waja wake na akaisifia haizungumzii elimu hiyo isipokuwa ni mnafiki au mwendawazimu, na ikawa yule mwenye kuipinga elimu na kuifanyia uadui na akatunga vitabu kwa ajili ya kutadharisha nayo na kuikataza ndiye mwanazuoni wa ulimwengu.
Msingi wa tano. Ubainisho wa Allah kuhusu vipenzi vyake, na kuwatofautisha wao na wale wenye kujifananisha nao miongoni mwa maadui wa Allah wanafiki na waovu, na inatosheleza ayah hii katika surat Al imran nayo ni kauli yake Allah akisema, {Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allah basi nifuateni mimi, nae Allah atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu }[3:31]
Na ayah katika suratul Maida, nayo ni qauli yake Allah, { Enyi mlio amini! Yule atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Allah atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda } [5:54]
Na ayah katika suratu Yuunus, nayo ni qauli yake Allah, {Tambueni kuwa vipenzi vya Allah hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika*Hao ni wale ambao wameamini na wakawa wanamcha Allah }[10:62-63]
Kisha likawa jambo mbele ya wengi wenye kudai wana elimu, ya kwamba ni miongoni mwa viumbe walioongoka na wenye kuhifadhi sheria ya kuwa hakika vipenzi vya Allah lazima wao waache kuwafuata mitume, na mwenye kuwafuata mitume sio katika hao vipenzi wa Allah(kwa madai yao).
Na lazima waache jihaad, yule atakae pigana jihad si katika wao, na lazima waache imaan na kumcha Allah, na yule atakae lazimiana na imaan na kumcha Allah si katika wao, ewe Mola wetu tunakuomba wewe msamaha na afya hakika wewe ni mwenye kuzisikia duaa.
Msingi wa sita. Kuzirudi(kuzipinga) shubuha ambazo ameziweka Sheitwan, kwa kuacha Qur’an na sunna, na kufuata rai na matamanio tofauti tofauti, nayo ni: hakika kwamba Qur’an na sunna havifahamu vitu hivi isipokuwa MUJTAHID, na huyo mujtahid anasifiwa na sifa kadha na kadha ambazo huenda hazipatikani sifa hizo kwa Abubakar wala Umarب, mtu asipokuwa hivyo *****
{Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, na wao hawaamini*Hakika sisi tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu * Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni*Na ni sawa sawa kwao wao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini*Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema}[36:7-11]
Mwisho na tunamshukuru Allah mola wa viumbe vyote, na swala ya Allah iwe juu ya mtume Muhammad, na juu ya familia yake na maswahaba zake na salamu zilizo nyingi mpaka siku ya malipo.
مرتبط