.NI ZIPI NYIRADI ZA KULALA ZILIZO THIBITI KUTOKA MTUMEﷺ?
-
NI ZIPI NYIRADI ZA KULALA ZILIZO THIBITI KUTOKA MTUMEﷺ?JIBU: Ayat kurus kutoka kwa abu huraira ameipokea bukhar.
Anapuliza katika mikono yake kisha anasoma {qul huwa Allah ahad,na qul audhubi rabi lfalaq na qul audhubi rabi nasi katika mikono yake kisha anapaka kile anachokiweza katika mwili wake na ananzia juu ya kichwa na uso wake na mwili wake wa mbele anafanya hivyo( mara tatu ) ameipokea bukhar kutoka kwa Aisha: hakika ya mtumeﷺ alikuwa pindi anapoliendea tandiko lake kwa kila usiku anakusanya viganja nyake kisha napuliza katika viganja vyake na anazisoma hizo sura katika viganja vyake…….. hadithi
* « بِاسْمِكَ اللهم أَمُوتُ وَأَحْيَا. وَإِذَا قَامَ قَالَ: الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا وَإِلَيْهِ النُّشُورُ
Kwa jina lako ewe Allah nakufa na ninakuwa hai na anapoamka anasema sifa njema zina msitahiki Allah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na kwake yeye tutakusanywa kutoka kwa hudheifa ibn yamani {6960} na Abi dhari {5837}amezipokea bukhar na muslim {4886}kutoka kwa albaraa wamesema alikuwa mtumeﷺ pindi anapoliendea tandiko lake. anasema……mpaka mwisho.
* « اللهمَّ أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ لَا مَلْجَأَ وَلَا مَنْجَا مِنْكَ إِلَّا إِلَيْكَ آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ وَبِنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ
Ewe Allah nimeisalimisha nafsi yangu kwako na nimeelekeza uso wangu kwako na nimeliegamiza jambo langu kwako na nimeegamiza kwako mgongo wangu hali ya kukupenda na kukuogopa wewe hapana marejeo wala sehemu ya kukimbilia kutoka kwako isipokuwa kwako nimeamini kitabu chako ambacho umekiteremsha na nabii wako ambaye umemtuma mwenye kusema maneno haya kisha akafa katika usiku wake atakuwa amekufa juu ya umbile la kisilam ameipokea Bukhar {5840} kutoka kwa baraa ibn azib *** amesema alikuwa mtumeﷺ anapoliendea tandiko lake analala kwa ubavu wake wa kulia kisha anasema maneno haya
* « بِاسْمِكَ رَبِّ وَضَعْتُ جَنْبِي وَبِكَ أَرْفَعُهُ إِنْ أَمْسَكْتَ نَفْسِي فَارْحَمْهَا وَإِنْ أَرْسَلْتَهَا فَاحْفَظْهَا بِمَا تَحْفَظُ بِهِ عِبَادَكَ الصَّالِحِينَ
Kwa jina lako ewe mola wangu nimeweka mbavu yangu na kwako wewe naiinuwa ikiwa kama utaizuia nafsi yangu basi irehemu na ikiwa kama utaituma basi ihifadhi kwa kile uanacho hifadhi kwacho waja wako wema .ameipokea bukhar{5845} kutoka abu huraira
* « اللَّهَ أكبر (أَرْبَعًا وَثَلَاثِينَ) والحمد لله (ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ) وسبحان الله (ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ)
Allah akbar ( mara thelathini na nne )na sifa njema zinamsitahiki Allah (mara thalaathini na tatu ) na ametakasika Alllah (mara thelaathini na tatu) hakika kufanya hivyo ni bora kuliko mtumishi
Ameipokea bukhar{2881}na muslim kutoka kwa aliy: kutoka kwa mtumeﷺ akaitaja hadithi hii…..
*« اللَّهُمَّ رَبَّ السَّمَوَاتِ وَرَبَّ الأَرْضِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ رَبَّنَا وَرَبَ كُلِّ شيء فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوَى وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ وَالْفُرْقَانِ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شيء أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شيء وَأَنْتَ الآخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَىْءٌ وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَىْءٌ وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَىْءٌ اقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْرِ
Ewe Allah mola wa mbingu na mola wa ardhi na mola wa arshi mola wetu na mola wa kila kitu mpasuwaji wa mbegu na kokwa na mteremshaji wa taurat na injili na furqan najikinga kwako kutokana na shari ya kila kitu wewe ni mwenye kushika utosi wangu ewe Allah wewe ni wa mwanzo hakuna kabla yako chochote na wewe ni wa mwisho hakuna baada yako chochote na wewe ni wa wazi hakuna juu yako chochote na wewe umefichikana hakuna chini yako chochote tulipie sisi deni na tutajirishe kutoka na ufakiri” kutoka kwa abu huraira ameipokea muslim{2713}
* « الحمد لله الذي أطعمنا وسقانا وكفانا وآوانا فكم ممن لا كافي له ولا مؤوي»
Sifa njema ni za allah ambaye ametulisha na akatunywesha na akatutoshereza na akatupa makazi ni wangapi ambao kutosherezwa wala hawana makazi” ameipokea muslim{2715} kutoka kwa Anasi hakika ya mtume ﷺ alikuwa pindi anapo lielekea tandiko lake anasema ….. mpaka mwisho.
* « اللهمَّ خَلَقْتَ نَفْسِي وَأَنْتَ تَوَفَّاهَا لَكَ مَمَاتُهَا وَمَحْيَاهَا إِنْ أَحْيَيْتَهَا فَاحْفَظْهَا وَإِنْ أَمَتَّهَا فَاغْفِرْ لَهَا اللهمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ»
Ewe Allah umeiumba nafsi yangu na wewe umeifisha ni kwako wewe kufa kwake na kuwa hai kwake ikiwa kama utaipa uhai basi ihifadhi na ikiwa kama utaifisha basi isamehe ewe Allah hakika mimi nakuomba afya” ameipoea muslimu {4887} kutoka kwa ibn omar kutoka kwa mtumeﷺ
* « اللهمَّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ عِبَادَكَ »( ثَلَاثَ مِرَارٍ ).
Ewe Allah nikinge mimi na adhabu yako siku utakapo wafufua waja wako { mara tatu} kutoka kwa hafswa mke wa mtumeﷺ hakika ya mtumeﷺ alikuwa pindi anapotaka kulala anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake kisha anasema dua hii. Ameipokea Abu daud {4388}na hadithi hii iko katika sahihi musinad
* « اللهمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِوَجْهِكَ الْكَرِيمِ وَكَلِمَاتِكَ التَّامَّةِ مِنْ شَرِّ مَا أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ اللهمَّ أَنْتَ تَكْشِفُ الْمَغْرَمَ وَالْمَأْثَمَ اللهمَّ لَا يُهْزَمُ جُنْدُكَ وَلَا يُخْلَفُ وَعْدُكَ وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ سُبْحَانَكَ وَبِحَمْدِكَ».
Ewe Allah hakika mimi najikinga kwa uso wako mkarimu na maneno yako aliyokamilika kutokana na shari ya kile ambacho wewe ni mwenye kushikilia utosi wake ewe Allah wewe unaondoa madeni na madhabi ewe Allah halishidwi jeshi lako na haukhalifiwi ahadi yako na hanufaishi mwenye utukufu kwako wewe ndo unatoka utukufu utakasifu ni wako na kuhimidiwa ni kwako kutoka kwa aliy kutoka kwa mtumeﷺ kwamba yeye alikuwa akisema dua hii wakati wa kulala kwake . ameipokea abu daud{439} na hadithi hii iko katika sahihi musinad
* « الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي كَفَانِي وَآوَانِي وَأَطْعَمَنِي وَسَقَانِي وَالَّذِي مَنَّ عَلَيَّ فَأَفْضَلَ وَالَّذِي أَعْطَانِي فَأَجْزَلَ الْحَمْدُ لِلَّهِ عَلَى كُلِّ حَالٍ اللهمَّ رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيكَهُ وَإِلَهَ كُلِّ شَيْءٍ أَعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ
Sifa njema ni za Allah ambaye amenitosheleza mimi na akanipa makazi na akanilisha na akaninywesha na ambaye amenemesha juu yangu na kazidisha fadhila zake na ambaye amenipa mimi akakithirisha sifa njema ni za Allah juu ya kila hali ewe Allah mola wa kila kitu na mumiliki wake na mwabudiwa wa kila kitu najikinga kwako kutokana na moto”kutoka kwa ibn omar *** hakika ya mtumeﷺ alikuwa akisema wakati wa kulala kwake …….. mpaka mwisho
Ameipokea Abu daud {4399}na hadithi hii iko katika swahihi musinad
UTANGULIZI WA TAJUWIDI.
مرتبط