WATAHADHARINI MAKHAWARIJI
NDUGU ZENU KATIKA MASJID ALBANI YA ELIMU ZA HADITHI DAR ES SALAAM
بسم الله الرحمن الرحيم
HUU NI UBAINIFU KWA WATU
Kila sifa njema ni zake Allah mwenye kuhimidiwa na swala na salamu ziwe juu ya mtume wetu ﷺ na ahli zake na maswahaba wake na yule mwenye kumfuaata;
Ama baada ya utangulizi huu, hakika miongoni mwa aliyoneemesha Allah juu yetu baada ya neema ya uislamu na sunna ni neema ya kutafuta elimu ya kisheria, elimu ya kitabu na sunna.
Na kwa hakika Allah ametuwepesishia neema nyingi katika Darul hadith iliyopo masjid Albany rahimahullah tunamshukuru Allah juu ya neema hizo.
Amesema Allah mtukufu “Na hamna neema yoyote mliyo nayo isipokuwa inatoka kwa Allah.”[suratun-nahli 53]
Na miongoni mwa hizo neema ni;
-
Kufuata quran na sunna na kuifanyia kazi, ahlu sunna waljamaa wanalingania katika haki na uislamu sahihi ambao quran na sunna vimeuashiria. Na miongoni mwa yanayolinganiwa na Ahlu sunna ni;
-
Kumpwekesha Allah na kumuabudu peke yake, yeye ndiye aliyewaumba waja na akawaumbia wao yote yaliyomo ardhini.
-
Kufuata kitabu na sunna juu ya ufahamu wa wema waliotangulia, na tunataraji Allah aliyetukuka atufishe katika quran na sunna.
-
Kumpwekesha Allah na kumuabudu peke yake, yeye ndiye aliyewaumba waja na akawaumbia wao yote yaliyomo ardhini.
-
Kushikamana na sunna, na tunatahadharisha kutokana na matamanio ya nafsi na makundi ambayo yanasababisha migongano na mipasuko katika dini.
-
Tunalingania kuelekea katika elimu na subira juu ya elimu na kuifanyia kazi elimu sahihi na kuilingania katika elimu hiyo.
-
Tunalingania watu wote kuelekea katika katika haki, hamna kufaulu kwa nyumati zote na kwa watu wakubwa na wadogo, wanaume na wanawake isipokuwa kwa elimu yenye manufaa na matendo mema na kurejea kwenye dini ya mlezi wa mbingu na ardhi.
-
Kutahadharisha kutokana na kutokuwatii viongozi na makundi ya kisiasa ambayo hamna nyuma yake isipokuwa misiba.
-
Na kwa ajili hiyo ni wajibu kukemea yale ambayo wanayoyafanya MAKHAWARIJI(wanaharakati) na DAESH(ISIS) na AL-SHABABU na BOKO HARAMU katika mauaji na kutoka katika twaa ya viongozi na kulipua mabomu na kukatakata viungo vya mwili na kuunguza na haya yote uislamu hauyakiri na wala Allah hayaridhii wala mtume wake na waumini, bali uislamu unawalingania watu kuelekea kwenye haki na upole na amani na imani na unawatoa watu kutoka katika giza na kufru na uadui.