«

»

sample matw

 

UJUMBE KWA ANAETAKA UISLAMU.

IMEANDIKWA NA

ABUL YAMAAN ADNAAN

AL-MASQARY

NDUGU MWISLAMU
Kila sifa njema zinamstahiki Allah tunamshukuru na tunamtaka msaada na tunamtaka msamaha na tunajikinga kwa Allah kutokana na shari za nafsi zetu na kutokana na matendo mabaya, mwenye kumuongoza Allah hakuna wa kumpoteza na mwenye kumpoteza hakuna wa kumuongoza na nashuhudia ya kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake hana mshirika, na ninashuhudia hakika ya Muhammad ni mja na ni mtume wake.
Hakika mwenye kuwafikishwa na Allah kwa uislamu na kushikamana na sunna za mtume ﷺ atakuwa ameongozwa katika dini ya Allah ya haki na neema yake ya uhakika na fadhila zake kubwa kwa yule Allah ataekaemtakia kheri.
Anasema Allah mtukufu, “Hakika dini ya haki mbele ya Allah ni uislamu”. na anasema Allah mtukufu, “Na nimeuridhia uislamu kuwa ndio dini yenu”. na anasema, “Na atakaetafuta dini isiyokuwa ya uislamu haitokubaliwa kutoka kwake dini hiyo”.
Na katika sahihi muslim kutoka kwa Abu Hurairah اkutoka kwa mtume ﷺ amesema “Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo mikononi mwake hanisikii mimi yeyote katika umma huu, myahudi wala mnaswara[mkristo] kasha

akafa hali ya kuwa hakuamini kile nilichotumwa kwacho, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni”.

Uislamu ni dini ya Allah ya haki, mwenye kutafuta haki katika dini isiyokuwa hiyo, atakuwa amepotea na ameenda upande.

Ubora wa uislamu na mazuri yake na mepesi yake ni mengi, Nayo ni dini ya msamaha na huruma na tabia njema na kujizuia na ukarimu na utukufu na murua, kila kheri ipo katika dini hiyo na mazuri yake ni mengi hayahesabiki.

Kutoka kwa Abu Hurairahا anasema; amesema mtume ﷺ“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake anakaribia kuteremka kwenu Issa mwana wa Maryam hali ya kuwa ni hakimu muadilifu atavunja misalaba na ataua nguruwe na ataondoa kodi na itaenea mali mpaka hatoikubali yeyote. Ameitoa muslim.[155]

Uislamu ni dini yenye kubaki mpaka siku ya qiyama, kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah ا anasema nimemsikia mtume ﷺ anasema, “Halitoacha kundi katika umma wangu linapigana katika haki hali ya kuwa ni lenye kudhihiri mpaka siku ya qiyama” akasema “kisha atashuka Issa mwana wa Maryam atasema kiongozi wao “njoo utusalishe” atasema “hapana hakika baadhi yenu ni viongozi wa baadhi, takrima ya Allah kwa umma huu”. Ameitoa Muslim.[156]

Nayo ni dini nyepesi, kutoka kwa Abu Hurairahاkutoka kwa mtumeﷺ

amesema, “Hakika dini ni nyepesi, wala hatoweka yeyote ugumu katika dini isipokuwa itamshinda, hivyo fanyeni kati na kati na ikaribieni haki na toeni bishara njema na takeni msaada kwa wakati wa asubuhi na jioni na sehemu ndogo katika usiku. Ameitoa Bukhari Allah amrehemu.

Na atakaekufa katika uislamu atakuwa amefaulu, imepokewa kutoka kwa Uthman ا amesema, amesema mtume ﷺ “yeyote atakaekufa hali ya kuwa anajua kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ataingia peponi”. Ameitoa Muslim[26]

Na yeyote atakaeslimu, Allah humsamehe madhambi yake yote, kutoka kwa Amru Ibn Aasw ا, nilimjia mtume ﷺ nikamwambia, kunjua mkono wako wa kulia ili nikupe baia’a[kiapo cha utiifu], akakunjua mkono wake, nikakunja mkono wangu, akasema mtume ﷺ una nini wewe Amru? amesema Amru nikasema “nataka niweke sharti” akasema mtume ﷺ unashurutisha jambo gani? nikasema “nisamehewe mimi” akasema “hivi hujui kuwa uislamu unavunja yaliyo kabla yake na hijra inavunja yaliyo kabla yake na hijja inavunja yaliyo kabla yake”. Ameitoa Muslim.

Nayo ni dini ya kufaulu, kutoka kwa Abdullah Ibn `Amri Ibnil `Aasw ا hakika mtume ﷺamesema,

“Amefaulu mwenye kusilimu na akaruzukiwa chenye kutosheleza, na Allah akamkinaisha kwa alichompa. Ameipokea Muslim[1054]

Ewe mja jitahidi kwa ajili ya dini yako na jisalimishe utasalimika duniani na akhera na muamini Allah mlezi wako utapata amani na furaha na utaishi maisha yalio mazuri.

Ewe mwenye kutaka uislamu jua ya kuwa hutojisalimisha uislamu anaouridhia Allah na mtume wake na wala hutosalimika kutokana na moto wa Allah wenye kuunguza isipokuwa kwa kuslimu uislamu wa mtume wa Allah na umfuate mtume ﷺ.

Hivyo tahadhari kutokana na kuslimu na ukaenda na masufi, washirikina ambao wamejifananisha na manaswara.

Na ole wako kuslimu na ukaenda na mashia marafidhwa ambao wanawatukana maswahaba wa mtume wa Allah na wanajifananisha na mayahudi.

Na ole wako kuslimu uislamu wa mahizbi[watu wa makundi] na watu wa bidaa ambao wameibadilisha dini na wamezusha katika dini hiyo.

Na yeyote mwenye kutaka uokovu kutokana na adhabu za Allah na hasira zake basi juu yake kushikamana na uislamu na sunna kama alivyosema Allah aliyetukuka, “Hakika walio igawa Dini yao na wakawa makundi makundi, huna uhusiano nao wowote. Bila ya shaka

jambo lao liko kwa Allah…’’ [Al an-aam]

Na amesema Allah aliyetukuka “ Sivyo hivyo! Yeyote anayeelekeza uso wake kwa Allah na hali ya kuwa ni mwenye kufanya wema, basi anayo malipo yake kwa Mola wake Mlezi, wala hakuna khofu juu yao na wala hawahuzuniki.” [Al baqarah:112]

Na amesema mtume wetu ﷺ “yeyote atakaefanya tendo lolote katika dini hii ambalo halina juu yake amri yetu, basi tendo hilo ni lenye kurudishwa.” Ameipokea Bukhari na Muslim kutoka kwa Aisha ل

 

 

 

Na kila sifa njema zinamstahiki Allah mlezi wa viumbe wote

 

 

 

KITABU NA SUNNA KWA UFAHAMU WA WEMA WALIOTANGULIA.

 

 

MARKAZ SHEIKH ALBANY

أضف تعليقاً

لن يتم نشر عنوان بريدك الإلكتروني. الحقول الإلزامية مشار إليها بـ *

يمكنك استخدام هذه HTML الدلالات والميزات: