«

»

WALIOHARAMISHWA KUOLEWA KATIKA WANAWAKE.

بسم الله الرحمن الرحيم

WALIOHARAMISHWA KUOLEWA KATIKA WANAWAKE.

Walioharamishwa kuolewa katika wanawake ni aina kumi na tano (15).

 

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ مِنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُمْ مِنْ نِسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَإِنْ لَمْ تَكُونُوا دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَنْ تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا

 النساء: ٢٣

Amesema Allah, “Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika Allah ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.” Surat nisaa 23

  1. AKINA MAMA. Amesema Allah, “Mmeharimishiwa mama zenu..)

  2. Na wanaokusudiwa ni mama aliyekuzaa na mama wa baba na kwenda juu na mama wa mama kwa kwenda juu (yaan bibi na bibi wa bibi)

  3. MABINTI ZENU.

  4. Nao ni mabinti zenu mliowazaa kutoka kwa wake zenu au mabindi waliozaliwa kutoka kwa watoto wenu wa kiume au waliozaliwa kutoka kwa mabinti zenu(yaan wajukuu)n na kushuka (yaan watoto wa wajukuu.)

  5. DADA ZENU.

  6. Nao ni wale wanawake wanaozaliwa pamoja nawe ima kwa upande wa baba na mama au kwa upande wa baba tu au kwa upande wa mama tu wote hao ni dada zako.

  7. SHANGAZI ZENU.

  8. Nao ni wale ndugu zake baba wa kike sawasawa wawe wamezaliwa tumbo moja na baba yako au upande wa baba tu au upande wa mama tu.

  9. MAMA WAKUBWA AU WADOGO.

  10. MABINTI WA KAKA ZENU.

  11. Nao ni katika upande wowote , sawasawa akawa binti wa kaka yako upande wa baba na mama au binti wa kaka upande wa baba tu au upande wa mama tu, na anaingia binti wa kaka ambae mmenyonya nae ziwa moja ima awe mtoto wa huyo mama au amenyonya kwake tu.

  12. MABINTI WA DADA ZENU.

  13. Nao ni katika upande wowote , sawasawa akawa binti wa dada yako upande wa baba na mama au binti wa dada upande wa baba tu au upande wa mama tu, na anaingia binti wa dada ambae mmenyonya nae ziwa moja ima awe mtoto wa huyo mama au amenyonya kwake tu.

  14. MAMA ULIENYONYA KWAKE.   

  15.  

  16. Nae ni yule mwanamke ulinyonya kwake mara tano za kushibisha mida tofauti tofauti, huyu hutoruhusiwa kumuoa wala mama yake au bibi yake kwasababu wote ni mama zako.

  17. DADA ULIYONYONYA NAE.

  18. Nae ni kila mwanamke ambaye amekunyonyesha mama yake au amenyonyeshwa na mama yako au umenyonya nae kwa mwanamke mmoja.

  19. MAMA WA WAKE ZENU.

  20. Nae ni mama yake mke wako, ni haramu kwako kumuoa au bibi yake na kuendelea juu.

  21. BINTI WA MKE WAKO. NB; anakua haramu mama baada ya kumuoa binti yake tu, na anakua haramu binti baada ya kumuoa mama yake na kumuingilia.

  22. Nae ni binti aliezaliwa kwa mke wako kabla ya kumuoa wewe na hawi haramun kwako ila baada ya kumuingilia mama yake.

  23. WAKE ZA WATOTO ZENU.

  24. Nao ni wale walieolewa na watoto zenu au watoto wa watoto zenu. Wanakua haramu kwenu pale inapopita ndoa tu.

  25. WAKE ZA BABA ZENU.

  26. Wanawake walioolewa na baba zenu ni haramu kuwaoa na anaingia baba yake baba(babu) na kuendelea juu na pia baba yake mama na kuendelea.

  27. DADA WA MKEO. NB; SHEMEJI

  28. Nae ni haramu kuolewa nawe, ikiwa bado dada yake ni mke wako. Nae akifa dada yake au ukampa talaka na ikaisha eda itafaa kumuoa ndugu yake. Na huu ni uharamu wa wakati maalumu sio wa milele.

  29. WANAWAKE WALIO OLEWA.

  30. Mwanamke yeyote alieolewa ni haramu kuolewa na mtu mwingine kwasababu ni mke wa mtu tayari, isipokua atakapotoka katika himaya yake(yaani atakapopewa talaka).

أضف تعليقاً

لن يتم نشر عنوان بريدك الإلكتروني. الحقول الإلزامية مشار إليها بـ *

يمكنك استخدام هذه HTML الدلالات والميزات: